Monday 2 March 2015

TUWAJALI WABUNIFU WETU.

  Ubunifu katika maisha ya kawaida ni jambo muhimu. Hii itakuwezesha kuzikabili changamoto mbalimbali zinazokukabili. Matatitizo mengi katika maisha huhitaji mtu kuwa ni mbunifu ili tu aweze kutatua. Hivyo ni muhimu kujua jinsi changamoto na jinsi ya kuzikabili.
  Changamoto zilizo nyingi zikikabiliwa kwa namna nzuri mara zote huwa na faida chanya kwa mpambanaji, hivyo ni busara sana kuzichukulia changamoto zetu kama njia ya kuinukia hatua bora zaidi ya kimaisha.
Ubunifu wa kuzalisha mali au kuimarisha jambo fulani ni muhimu kwani huweza kuwafaa hata watu wengine wa pembeni. Jambo bora hapa ni kuwa mbunifu mzuri ili uweze kuinua pato lako na la taifa.
nikiendelea zaidi naweza kusema kuna aina mbali mbali za ubunifu.
Huu unaweza kuwa ni ubunifu wa Kuzalisha mali
Utengenezaji wa bidhaa au vitu mbalimbali
Ubunifu wa kuhudumia jamii katika sekta fulani n.k.
Kwa aina zote hizi za ubunifu nitazingatia zaidi ubunifu wa kutengeneza vitu mbalimbali
 mf. Mashine kama vile za kuzalisha umeme,magari, ndege na vitu vingine vingi.
Tanzania kama nchi iliyobarikiwa imekuwa na tatizo kubwa la ajila. serikari inajitahidi kukabiliana na tatizo hili lakini bado limekuwa likisumbua vijana.
  Vijana wengi wamekuwa wakiishia kuilaumu serikali kwa kushindwa kuwapa ajira,ili hali wengi wao hata hajishugulishi ingawaje wapo wachache wanaojitahidi kuwa wabunifu ili kuweza kuzikabili changamoto zao kimaisha kama nilivyo sema mwanzo.
Naamini jitihada hizi za vijana wachache zinaweza kufanya mambo makubwa kwa Taifa zima, hii inaweza pia kuwa ni kupunguza wimbi la ajira. Ubunifu wa vijana hawa hujumuisha pia utengenezaji wa bidhaa hali ambayo ni rahisi sana pia kuajiri vijana wengine katika uzalishaji huo.
  Ukiangalia vizuri na kama utakuwa na imani kama yangu ni hakika kuwa ubunifu huu wa kuteneneza bidhaa na machine mbalimbali unaweza kuwa ni mwanzo wa viwanda vidogo vidogo na vikubwa hapa nchini. Na endapo ndio hali ikawa hivyo inamaanisha kuwa ajira zitaongezeka kwa kiasi kikubwa nchini.
  Lakini kitu ambacho nimekuwa nikishuhudia ni kuachwa bila matumaini yakuendelea mbele kwa wabunifu hawa. wengi wamekuwa wakijitokeaza wakiwa na mawazo mapya mazuri lakini huishia kupongezwa au kusifiwa bila msaada. Wapo waliojitokeza wakionesha jinsi walivyo tengeneza gari lao huko Dodoma mwaka fulani lakini leo siwasikii, wapo waliotengeneza mashine za kufua umeme  lakini ni wao tu hakuna uwezeshaji wowote.
  Serikali yetu imekuwa ikitumaini sana katika viwanda vya nchi za nje ikasahau kuwa hata vile  viwanda visingekuwa vile kama isingekuwa serika za nchi husika kuthamini vipaji na uwezo wa raia wao. Nchi zilizoendelea kama vile Marekani na nchi nyingine zimekuwa zikithamini sana ugunduzi wa raia wake, inakuwaje nchi maskini kama tanzania inashindwa kuthamini kwa dhati vipaji vya Watanzania! 
  Endapo tanzania Itakita zaidi katia kuimarisha na kuviangalia kwa umakini ubunifu wa watanzania basi huo utakuwa mwanzo mzuri wa kuwa na viwanda vyetu wanyewe, si jambo lakufurahisha kuona Hata vitu vidogo tunasubiri vitengenezwe na wenzetu ndipo na sisi tutumie, ili hali na sisi tunaweza kufanya hivo.
  Watu wengi wamekuwa wakijiuliza viwanda vilivyokuwezamani siku hizi vimekuwa vikididimia na kupotea kabisa badala ya kuendelea kuimarika.tulikuwa na viwanda vya nguo, matairi ya magari, vyuma na vingine vingi siku hizi viko wapi? Ni wakati wa sisi kukubali kubadilika na kuwa tayari kufanya jambo kwa ajili ya Tanzania yetu.
  Kwa maoni yangu zaidi ni vizuri kuwa na taratibu nzuri zitakazo wawezesha wabunifu wetu kuweza kunufaika na kuendelea mbele zaidi.Kuwa na mashirika yatakayo simamia maendeleo na kushirikiana nao katika kuzikabili changamoto zao. Zaidi kuwaunganisha na kwawzesha kwa kuwapa vifaa vitakavyo weza kutimiza ubunifu wao

No comments:

Post a Comment

Featured post

Nafaka kwa uchumi na afya zetu pia