NAFAKA NA FAIDA ZAKE KIAFYA NA KIUCHUMI

Tunaposema nafaka tunamaanisha bidhaa zitokazo mashambani, hapa tukijumlisha mazao kama vile
 Mahindi
Nafaka kiafya na Kiuchumi Ngano,Viazi ( Vitamu na Mviringo)

 Ulezi, Mchele, Mtama Mboga mboga za majani mfano figiri, mchicha, nk. Pia kuna matunda kutoka mashambani mfano maembe nanasi machungwa, nyanya, parachichi na matunda mengine mengi

 Na bidhaa nyingine unazozifahamu.
bidhaa hizi kutoka mashambani zimekuwa zikitumika kwa matumizi mbalimbali majumbani mwetu,mahotelini, katika nyumba za wageni n.k.

Matumizi ya matunda ni pamoja na kutengeneza juisi au usindikaji wa pombe mfano ndizi hutumiwa na baadhi ya maeneo kutengeneza pombe.


Kuna aina nyingi sana za vyakula ambazo zimekuwa zikipatikana kutoka katika bidhaa hizi za mashambani, mfano wa vyakula hivyo ni kama vile

 MAHINDI_Ugali, uji, lishe, pombe.
MCHELE- Wali, vitumbua nk.
VIAZI-- Chipsi, Viazi, Clips,nk.

MTAMA.
DENGU hizi hutumika pia kutengeneza bagia

    Baadhi ya bidhaa hizo kutoka mashambani pia hutumika kutengeneza vinywaji vya aina mbali mbali mfano pombe za kienyeji.

    Endapo kama unaweza kuwa mbunifu juu ya utengenezaji wa vyakula vitokanavyo na bidhaa hizi za mashambani unaweza kuifanya jamii ikutegemee katika kujipatia mahitaji yake ya bidhaa hizi mfano mikate.
Hii inawea kuwa ni moja ya njia bora ya kujiajili na hivyo kuondokana na tatizo la ajira.
   Katika baadhi makala zetu zitakazofuata tutaangalia baadhi ya mapishi ya bidhaa hizi, pia tutajifunza utengenezaji wa juisi mbalimbali kutoka katika mazao hayahaya, huku tukiangalia na faida zake kiafya, hivyo nikusihi usiridhike kupitwa na na kile tutakachokuwa tunajifunza

     Pamoja na ajira pia vyakula hivi vimekuwa na faida zake katika miili yetu pindi tunapotumia kwa ufanisi, tukianzia na Mboga za majani na matunda, nafaka kama ngano, mahindi nk, alizeti na nazi yaani vyakula vyenye mafuta.
     Kwa ufupi sana hebu mimi na wewe tutazame baadhi tu ya faida au kazi za vyakula hivyo kiafya tukianza na Vyakula vyenye Vitamin.
    Vyakula vyenye Vitamin kwa wingi baadhi tu ni hivi vifuatavyo. 

Matunda
               





 fenesi, parachichi, karoti, nyanya, maembe,


Mboga za Majni,
 Mchicha, sukumawiki, matembele, spinachi, mnafu, kabeji, majani ya kunde au maboga, ya maharage,majani ya muhogo, pilipili hoho.



Vitamini ni muhimu sana kwa ajili ya afya ya macho, utando na ngozi, pia vitamini husaidia mwili kuweza kupambana na magonjwa madogo madogo ya mwili kwa kuimarisha kinga ya mwili, Vitamini hasa vitamini B12 husaidia kuimarisha mfumo wa neva za fahamu, kutengeneza DNA mpya na seli nyekundu za damu. 
Nafaka

Baada ya kuangalia faida za vitamini ipatikanayo katika mazao ya mashambani pia tunaweza kuangalia Baadhi ya faida za wanga na mafuta.
      Tukianzia na wanga, vyakula vyenye wanga kwa kiasi kikubwa ni kama vile mtama, uwele, Ngano, mahindi, magimbi, 
     pia hupatikana kwenye  viazi vitamu, ndizi,asali n.k. 


Katika mwili wa binadamu wanga  kiufupi tu,
Ni chanzo kikubwa cha nishati mwilini.

Mafuta
Vyakula vyenye mafuta kwa wingi ni
  1. Parachichi, alizet, ufuta,
  1. Karanga, Nazi,pamba,
  1. Zaituni

    Faida za Mafuta Katika Mwili wa Binadamu,

  1. Ni chanzo kizuri cha nishati mwilini.
  2. Mafuta husaidia uyeyushaji wa vitamini na hivyo hufyonzwa (Vitamini) kirahisi mwilini.
  3. Mafuta pia husaidia katika kulainisha ngozi zetu
  4. Pamoja na hayo na mengine mengi mafuta husaidia kuongeza ladha ya chakula.
Mafuta yanafaida nyingi sana kiafya hivyo tujaribu kuyatumia kwa kiasi kwani kuzidisha pia kuna madhara yake.


        

Lengo la kuandika makala hii si kukuelimisha juu ya faida za vyakula hivi kiafya tu bali pia, Lengo langu hapa ni  ubunifu wa ajira, yaani kupitia nafaka hizo, matunda kwa pamoja tuone tunatengeneza au tunabuni kitu gani cha kuifaa jamii yetu kupenda na hivyo mimi na wewe kupata chochote.Na pia kujipatia chakula chako binafsi mara baada ya kuwa umeweza kufahamu kwa uchache faida za vyakula hivi. Hivyo naomba nikukaribishe ndugu yangu, rafiki yangu tujifunze pamoja naomba ushiriki wako unapoisoma makala hii, tuelimishane zaidi.



Asante twende zetu pamoja. nikuombe usikose kuniachia maoni yako hapa chini.


No comments:

Post a Comment

Featured post

Nafaka kwa uchumi na afya zetu pia